JINSI YA KUDEAL NA MPENZI WAKO ANAETEXT MWANAUME MWINGINE

Habari Yako Mpenzi Msomaji!

Katika Zama Hizi Hasa Katika Ukuuaji Wa Utandawazi na Teknolojia Vimesababisha Changamoto Nyingi Katika Mahusiano.

Changamoto moja wapo ni Mwanamke(Mpenzi Wako) Kuwa Busy Akichati Na Wanaume Wengine Hio Ni Mojawapo ya changamoto za mahusiano katika zama hizi za teknolojia Tena mara nyingi hutokea ata mbele yako unakuta mwanamke yuko busy akicheka na kuendelea kutuma meseji kwa wanaume katika simu yake,Hii Mara nyingi hupelekea hali ya sintofahamu na wivu wa kimapenzi kuzidi kwa mwanaume

Leo Ewe Mwanaume Nimekuletea Suluhisho la tatizo lako unalolipata katika mahusiano Yako na mwanamke wako bila ya kuharibu mahusiano Yenu.Ungana nami katika somo hili fupi!


Mahusiano Yoyote hayatodumu Bila WENZA kuwa waazi kwa kila mtu


Mbinu Za Jinsi Ya Kudeal Na Mpenzi Wako Anaetext Mwanaume Mwingine.

1.Tambua Uhusiano Na Huyu Mwanamke Ni upi?

Kabla hujaanza kufata hatua hizi,tambua kwanza uhusiano wako na uyu mwanamke ni upi namanisha nini katika hili?

Wanaume wengine wanaweza kuchukulia swala hili zito kiundani na huku uhusiano wake na mwanamke huyu si wa kufaana na kudumu bali ni kutimiza haja zake binafsi.

Kama hauna malengo na huyu mwanamke kwa siku za usoni basi njia hizi sio mbadala kwako mwache aendelee kuchati na mwanaume aoneya ana malengo na yeye.

2.Je Ushakutana na Huyo Mwanaume?

Kama uko kwenye uhusiano wa nguvu na huyu mwanamke natumai utakuwa ushakutana na baadhi ya marafiki zake huyu mwanamke wako.

Je huyu mwanaume anaechati nae unamfahamu? Swala hapa ni kujua kama huyu mwanaume unamfahamu au ushawahi kumsikia katika maongezi ya mwanamke wake japo alishamtaja au ushamsikia anawasiliana nae!

3 Usipandwe na hisia.

Unamwona mpenzi wako akimtext huyu mwanaume mara kwa mara na haujapendezwa. Lakini pia wakati ambapo unamwona anachat naye usionyeshe hisia zako. Kama umekasirishwa usimwonyeshe. La kufanya ni kuwa unaweza kumuuliza huyo ni nani anaongea naye na umsikilize kila kitu ambacho atakuambia.

4 Usirukie majibu.

Akikueleza kila kitu kuhusiana na huyu mwanaume hupaswi kurukia kumwambia kuwa anakucheat ama anakuendea kinyume. Hili ni kosa kuu ambalo mwanaume aliyekamilika hapaswi kufanya kamwe.

5 Kusanya uhakikisho.

Wakati umeona kuwa mpenzi wako anachat na mwanaume mwingine, lazima ufanye utafiti umsome kila reaction ambayo anakuwa nayo. Je, tabia yake imebadilika? Je, siku hizi hapendi kuspend time na wewe, ama je anaficha simu yake ama amebadilisha password? Haya ndio maswali lazima uthibitishe kabla kurukia hatua yeyote ile.

6 Tambua kati ya rafiki na zaidi ya rafiki.

Kila mtu anakuwa na rafiki yake wa jinsia ile nyingine. Na huwa tunajua kutofautisha kati ya rafiki na ‘zaidi ya rafiki’. Ni rahisi kugundua kemia ya kimapenzi wakati ambapo watakuwa wanaongea pamoja ama wakirushiana texts. Jambo hili haliwezi kufichika.

7 Usimwonyeshe wivu mbele yake.
Ukimwona anaendelea kutext na mwanaume huyu, lile na kuepuka ni kutomuonyesha wivu. Hakikisha huonyeshi kuwa unaona wivu. Wanawake wengi hawapendi tabia za mwanaume mwenye wivu. Unaweza kuachwa haraka ukiwa na tabia kama hii.

8 Baada ya kuongea naye, soma reaction zake.

Mwelezee kuwa hupendi tabia yake ya kutext na wanaume hivi hivi kwa kuwa mwishowe inaweza kuleta matatizo katika relationship yenu. Ikiwa huyu ni mwanamke msikivu, basi ataitikia mwito wako na anafaa kupunguza kuchat na huyu mwanaume.

Iwapo unaona anakupuuza, basi lazima kuna matatizo kati yenu wawili. Hali kama hii atakuwa anakuonyesha ishara ya kuwa wewe hauna thamani ya zaidi kumliko huyu anayechat naye.

9 Kutana naye.

Ok, kama umegundua kuwa anakucheat na huyu mwanaume basi haina haja ya kukutana naye. Lakini kama ni rafiki yake tu mbona usimeet na yeye umjue zaidi? Kukutana naye kutakupa fursa ya kujua hadhi ya urafiki wa wawili hawa.

10 Unahitaji kubadilika.

Kama huyu mwanaume ni rafiki yake wa kweli basi ujue hataenda popote. Na usitarajie mabadiliko yeyote. So la kufanya hapa nikujikubali na kufanya juhudi za kuondoa woga na wasiwasi kuhusiana na huyu mwanaume. Kumbuka ya kuwa si kila mwanaume atakaye kuwa naye inamaanisha kuwa analala naye ama anamtamani kihisia.

11 Usimwambie akatize mawasiliano.

Iwapo ni marafiki wa kawaida na huyu mwanaume basi haina haja ya kumwambia akatize mawasiliano. Ni marafiki tu na hakuna la ziada. Lakini kama unaona kuwa anakuwa interested zaidi na huyu mwanaume kukuliko basi unapaswa umwambie mambo mawili. Aidha akubali kukatiza mawasiliano na huyu mwanaume ama ukatize mahusiano na yeye. Lazima achague moja.

Mwisho ni kuwa lazima ufahamu kwamba kuwa katika mahusiano si rahisi. Wengi hujipata wamependa sehemu ambayo haiwafai na wengine bado wanasumbuka kupata angalau mwanamke mmoja amuite mpenzi. So ukiwa katika mahusiano na mwanamke hakikisha kuwa unalinda mapenzi yenu.

Usisahau kushare na kutoa maoni yako hapa chini

Post a Comment

0 Comments